ENEWZ AFRICA | Waziri Nape ameandika hiki baada ya kuona habari zake mitandaoni
February 13 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zilisambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinazodaiwa kutaka kumgombanisha yeye na baadhi ya viongozi wenzake wa serikali.
Kupitia ukurasa wake wa Tweeter Waziri Nape aliandika…>>> ‘Tujifunze kusoma biblia, Nasoma masomo ya Mwakasege watu wanachukua na kutafsiri watakavyo kwa faida zao.Nimesikitishwa sana. Si SAWA!‘
Hii imekuja mara baada ya usiku wa February 14 2017 kupitia ukurasa wake huohuo Waziri Nape alinukuliwa kwa kaundika >>>’Ujinga ni mzigo mkubwa sana!! Omba busara ya Mungu kwa kila jambo kuliko utajiri na kiburi!‘
Huku akiambatanisha na kipande cha video cha Mchungaji Christopher Mwakasege aliyenukuliwa akisema ‘Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu, sio kwamba hana akili bali amepungukiwa‘
Kwa ufupi ni kwamba Waziri Nape amesema alichokiandika hakijamlenga na wala hajakiweka kwa makusudi yoyote yenye nia ya kumsema kiongozi yeyote, ni utaratibu wake kusoma masomo ya Mwakasege.
No comments: