SPORTS EXTRA | Hizi ni taarifa nzuri kwa mashabiki wa Arsenal kuhusu mchezaji Hector Bellerin
Mchezaji wa klabu ya Arsenal Hector Bellerin baada ya kuumia katika mchezo wao dhidi ya Chelsea majibu ya vipimo vya MRI yametoka na kuondoa hofu kwa mchezaji huyo kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Bellerin alishindwa kuendelea na mchezo huo baada ya kugongwa na Marcos Alonso, hali ambayo ilizua hofu kwa wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wa Arsenal.
Majibu ya vipimo vya MRI alivyofanyiwa mchezaji huyo ambaye ni raia wa nchini Hispania, yameonyesha hana tatizo kubwa na tayari ameshapewa ruhusa ya kujumuika na wachezaji wenzake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Hull City.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 21, alitarajiwa kuwa sehemu ya wachezaji ambao wanaendelea na maandalizi ya kujiwinda na mchezo dhidi ya Hull City ambao utapigwa katika uwanja wa Emirates.
klabu ya Arsenal ilionyesha kuwa na wasiwasi wa mkukosa mchezaji huyo, na ilitoa tahadhari kwa mashabiki wote duniani kwa kusisitiza huenda Bellerin, akakaa nje kwa kipindi kirefu.
No comments: