ENEWZ AFRICA | DULLY SYKES-: NIMEJITAHIDI KUWAPATANISHA ALIKIBA NA DIAMOND PLATNUMZ NIMESHINDWA
Dully Sykes ni mmoja kati ya wasanii wakongwe na wenye heshima kubwa sana kwenye game ya music hapa Bongo. Heshima kuanzia kwa wadau na hata wasanii ambao wanafanya game kwasasa.
Licha ya heshima tu, Dully Sykes ni mtu wa karibu wa wasanii Alikiba na Diamond Platnumz. Wasanii ambao inatambulika fika wana upinzani mzito kuanzia kwenye kazi mpaka kwenye maisha ya kawaida.
Dully Sykes alitaka kutumia ukaribu wake huo na wawili hao pamoja na heshima ambayo wanampa kutaka kuwaweka karibu na ikiwezekana kumaliza tofauti zao kabisa.
Point ni kwamba mipango ya Dully Sykes imefeli kwa asilimia 100%. Dully Sykes Akiongea hayo kupitia kipaza cha CLOUDS FM na kuamua kuweka pause kwenye mchongo huo na kafanya mambo mengine labda atakuja kujaribu tena next time.
No comments: