Ni bora nikose vyote lakini sio wewe – Rayvanny
Msanii kutoka WCB, Rayvanny amemuandikia ujumbe mwanae Jaydan na kumueleza yeye ndio sababu ya kujituma kwake katika kazi na hayupo tayari kumkosa.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Rayvanny ameandika, “Mungu akukukuze mwanangu, katika mema na mafanikio katika maisha yako, wewe ni furaha yangu na pia wewe ndio sababu ya mimi kumwaga Jasho, nakufanya kazi kwa bidii kila siku. Ni bora nikose vyote lakini sio wewe Mwanangu. I LOVE YOU SON Jaydan,”.
Huyu ni mtoto wa kwanza kwa Rayvanny ambaye amezaa na mrembo Fahyma, pia hii ni picha ya kwanza kwa Rayvanny kumpost katika mtandao tangu mwanae azaliwe.
No comments: