Priyanka Chopra aoga mvua ya matusi mitandaoni
Muigizaji maarufu wa India anafanya kazi zake huko Holywood, Priyanka Chopra amekumbana na mvua ya matusi baada ya kuonekana kama alikuwa anamtega waziri mkuu wa India Narendra Modi wakati walipokutana kwa mazungumzo.
Kitendo cha kuonyesha miguu yake ikiwa wazi mbele ya kiongozi huyo kimeonekana kama amemkosea sana heshima.
Hata hivyo Priyanka alionekana kushindwa kuvumilia matusi na kejeli za mashabiki huko mitandaoni, ndipo alipoweka picha akiwa na mama yake mzazi, Madhu Chopra huku miguu yao ikiwa inaonekana.
“Legs for days….#itsthegenes with @madhuchopra nights out in #Berlin #beingbaywatch, ” ameandika katika picha hiyo.
No comments: