Namba 23 yaibua vita Jangwani
Hivi karibuni klabu ya Dar es salaam Young Africans imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajibu ambapo usajili huo umekuwa gumzo kwa wadau na mashabiki wa mchezo wa soka nchini.
Ajibu ambaye hutumia namba 23 mgongoni wakati alipokuwa akiitumikia klabu ya Simba ana kutana na mchezaji wa muda mrefu ndani ya kikosi cha Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye pia hutumia namba hiyo mgongoni mwake.

Mchezaji wa yanga anaevaa jezi namba 23 , Nadir Haroub ‘Cannavaro (wambele)
Mchezaji Ibrahim Ajib Migomba mwenye umri wa miaka 21 ameingia mkataba wa miaka 2 na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na hivyo usajili huo kuleta uchokozi baina ya mahasimu hawa wakubwa.
Mchezaji Ibrahim Ajib Migomba alipo kabiziwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kutokana na Uwezo wake ndani ya uwanja
Uchokozi wa usajili huo ni kutokana na uwezo wa mchezaji na umuhimu wake ndani ya klabu ya Simba licha ya timu hiyo kushindwa kumzuia kutosajiliwa na Yanga.
Kipaji alichojaliwa Ajib hakuna ubishi kwa mdau yeyote wa mchezo wa soka nchini.
Kipaji alichojaliwa Ibrahim Ajib kinamfanya kijana huyu mdogo kuandika namba 23 na jina la Ajib kuonyesha kuhusudu uwezo wa mchezaji huyo
BY HAMZA FUMO
No comments: