Ariana Grande kutunukiwa uraia wa heshima
Msanii wa muziki kutoka Marekani, Ariana Grande aliyekumbwa na mkasa wa kukatisha tamasha lake la ‘Dangerous Woman’ kufuatia mlipuko, anatarajiwa kupata uraia wa heshima.
Grande alikatisha tamasha lake baada ya kutokea mlipuko katika ukumbi wa Mancherster Arena, Jijini Manchester tukio liliotokea mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu 59.
Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la nchini Uingereza limeripoti kuwa Grande atapatiwa uraia wa heshima kutokana na mchango aliyoutoa kwa wahanga wa tukio la kigaidi katika mji wa Mancherster.
Msanii huyo atakuwa msanii wa kwanza kupata heshima hiyo. Mnamo Juni 5 mwaka huu alifanya tamasha lingine maalumu lililopewa jina la ‘OneLoveMancherster’ kwa ajili ya kuchangia na kufariji wahanga wa tukio.
No comments: