Kylie Jenner na Travis Scott waonyesha mapenzi mubashara
Kylie Jenner na rapper Travis Scott wameendelea kuonyesha mahusiano yao yanavyozidi kuimarika kila kukicha.
Wawili hao wameamua kuchora tattoo zinazofanana katika miguu yao.
Kupitia mtandao wa Snapchat, Jenner ameweka picha inayoonyesha akiwa amechora totoo ya kipepeo chini ya mguu wake wa kulia huku Scott akiwa amechora tattoo kama hiyo sehemu ya chini ya mguu wake wa kushoto.
Mchoro huo unaonyesha kuna kitu cha umuhimu kipo katika mahusiano ya wawili hao ambao wameanza kuonekana kuwa pamoja tangu mwezi Mei mwaka huu.
No comments: