Gabo nitatoa filamu zangu bure
Mkali wa filamu Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amefunguka kwa kudai ameamua kujitolea kufa na kupona ili tasnia ya filamu isonge mbele kwa kuleta mifumo mipya ambayo itawasaidia Watanzania kupata filamu zake bure na kwa urahisi.
Akiongea na Bongo5 jana muda mchache baada ya kuzindua filamu yake mpya ‘Kisogo’ iliyochini ya Kampuni yake ya Baridi Media, Gabo amedai ameamua kutoa sehemu ya maisha yake ili kuikomboa tasnia ya filamu ambayo imeonyesha kupoteza imani kwa mashabiki wa filamu nchini Tanzania.
“Mimi nimeamua kuikomboa tasnia ya filamu, unajua kuna wakati unafika lazima ukubali maneno ya watu ambao ni mashabiki wetu,” alisema Gabo. “Kwahiyo mimi binafsi nimeanza kutoa filamu fupi ambazo zitakuwa zikipatika katika App ya Uhondo, nimeanza na Kisogo, hizi filamu zimezingatia ubora ya kila kitu kuanzia picha, sauti, wahusika yaani kila ambacho kilikuwa kinazungumza mtandaoni kuhusu filamu,”
Aliongeza,”Kwa sasa filamu hizi fupi zitapatikana kupitia mtandao huo na kila mwenye simu ya mkononi anaweza kuzipata, part 1 utaangalia bure na part 2 utachangia pesa ndogo ili tuweza kuzalisha kazi nyingi zaidi. Lengo letu kila mtanzania aangalie filamu zetu na baadaye nataka kufanya bure kabisa ili kila mtanzania aangalie nini tunafanya kwa manufaa ya taifa hili,”
Muigizaji huyo amedai kwa upande wa filamu ambazo zimezoeleka ambazo wamekuwa wakizitoa kwenye mfumo wa (DVD) na kuziingiza sokoni hapendi kuzizungumzia kwa kuwa bado hazipo rasmi kwa serikali ndiyo maana kuna changamoto nyingi.
Filamu ya ‘Kisogo’ ni filamu ambayo ameshirikiana na malkia wa filamu Wema Sepetu.
No comments: