Aslay amtosa Alikiba
Msanii Aslay amefunguka na kuzikataa kabisa zile tetesi zinazosema kuwa hivi sasa yeye amepiga kambi kwa msanii Alikiba huku tetesi hizo zikidai huenda wakali hao wakaibuka na ngoma ya pamoja hivi karibuni.
Aslay alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live alizikataa tetesi hizo na kusema kuwa hazina ukweli wowote ule kwani yeye hana ukaribu na Alikiba wala hana ngoma yoyote ambayo amefanya na msanii huyo.
Mbali na hilo meneja wa Aslay Chambuso pia amepigilia msumali kuwa huo ni uzushi tu kwani msanii wake hana ukaribu na Alikiba na wala hajawahi kumzuia msanii huyo kujiunga na WCB kama ambavyo watu wengine wanadai.
No comments: