Yusuf Manji apiga hodi Mahakama Kuu
Mfanyabiashara maarufu
Yusuf Manji amewasilisha hati ya
kuiomba Mahakama Kuu iwaagize
maofisa Uhamiaji wamfikishe
mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa
mujibu wa sheria.
Manji yuko kwenye matibabu Hospitali
ya Aga Khan jiji hapa akiwa chini ya
ulinzi baada ya kuachiwa kwa dhamana.
Februari 20 mwaka huu, alipelekwa ofisi
ya Uhamiaji mkoa na kuhojiwa kwa
madai ya kuingia nchini kinyume cha
sheria.
Katika kesi hiyo wajibu maombi hayo ni
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa
Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam.
Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo
aliyefungua kesi ya maombi hayo,
anataka Mahakama iagize maofisa
uhamiaji na polisi kumfikisha
mahakamani ili iamue uhalali wa
kushikiliwa kwake na kuagiza aachiwe.
Katika hati ya maombi hayo, Ndusyepo
anadai kuwa alimtembelea mteja wake
hospitali ya Aga Khan Februari 17
mwaka huu na kukuta maofisa wa
Uhamiaji wakimsubiri mteja wake
wampeleke kwa ofisa Uhamiaji wa mkoa
kwa mahojiano dhidi ya tuhuma kuwa
siyo raia wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Ndusyepo, Manji ambaye
ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited
na Diwani wa Mbagala Kuu, Amedai
kuwa alitoa maelezo kwa maofisa
Uhamiaji na alirudishwa Aga Khan
ambako yupo chini ya ulinzi hadi leo.
No comments: