Breaking News
recent

"Hata kwa mganga nitakwenda" - Shilole

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shilole amefunguka na kuwataka vijana wa mjini ambao wanachukua 'Account' za watu mitandaoni waende kuiba kwenye taasisi za fedha na si kwenye mitandao ya jamii kwa kuwa huko hakuna fedha. 



Shilole amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kusema licha ya mwizi wake kumuachia account yake ya Instgram lakini anataka mtu huyo apatikane ili ikiwezekana afungwe kabisa kama fundisho kwa vijana wengine wanaofanya michezo hiyo kwani wamekuwa wakiwakwamisha na kuwarudisha nyuma wasanii.
"Mimi account yangu imesharudi saizi nashukuru Mungu ila nasema hao vijana wanaojifanya wao wamesomea IT na kuanza kuiba account za watu za mitandao ya jamii, wakaibe bank huko, kama wao wasomi wakaibe Ikulu, au wakatengeneze ndege huko, siyo mnakuja kuiba account za sisi wasanii sitawasaidia nini? Huko kwenye mitandao hakuna hela kama mnataka pesa nendeni bank huko. Mimi nasema hata kwa mganga wa kienyeji nitakwenda nimjue mtu aliyeiba account yangu ili afungwe tu iwe fundisho kwa vijana wengine" alisema Shilole
Shilole aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha account yake kuwa hacked kwa mwezi mzima imemuingizia hasara kubwa kwani ameshindwa kutoa wimbo wake mpya na ameshindwa kutangaza juu ya biashara yake ya chakula.
"Watu wanaweza kuona kama ni utani lakini mimi nipo serious hawa watu wanatupotezea focus yetu, mimi Instgram inanisaidia kutangaza muziki wangu, inanisaidia kutangaza biashara yangu ya chakula, mambo yangu mengi yamekwama kwa mwezi mzima toka huyo mtu ameiba account hiyo, halafu yeye alikuwa amekaa nayo hakuna anachofanya, nasema hawa watu wanaojifanya wanajua sana IT watumie vyema elimu zao kufanya mambo ya msingi" alisisitiza Shilole



No comments:


Powered by Blogger.