YANGA YAOMBA WANACHAMA WAICHANGIE, HALI NI MBAYA NI BAADA YA MANJI KUPATA MATATIZO
Uongozi wa Klabu ya Yanga umewataka wanachama na wapenzi wa timu hiyo kongwe hapa nchini kuichangia kwa hali na mali klabu hiyo katika kipindi hiki ambacho wamekumbwa na matatizo ya kifedha tangu Mwenyekiti wake Yusuf Manji apate matatizo.
Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa baada ya uongozi wa timu hiyo kuingia makubaliano na Kampuni ya Selcom kwa ajili ya kuendesha zoezi hilo maalum kwa ajili ya wanachama na wapenzi wa timu hiyo kuweza kuichangia timu yao.
Mkwasa amesema“Tumeingia makubaliano na Selcom kwa miezi mitatu ya kutuendeshea zoezi la wanachama wetu kuchangia fedha kwenye kipindi hiki ambacho tumekuwa na matatizo kidogo juu ya fedha ambapo makubaliano hayo yataendelea zaidi baada ya kuona faida ambayo tutaipata katika wakati huo.
Ameongeza kwa kusema “Wanachama watachangia klabu kwa njia ya mitandao ya simu kupitia huduma za kutuma fedha kwa njia ya kimtandao”alisema Mkwasa.
Mkwasa pia aliitaja namba ya kuchangia ni 150334 ambayo watumiaji wa mitandao yote ya simu za mkononi wanaweza kuitumia kuchangia klabu yao.
Kwa upande wake mwakilishi wa Selcom, Gallus Runyeta alisema kwamba wana matumaini zoezi hilo litafanikiwa sana na Yanga watanufaika.
“Sisi kama Selcom tunafurahi kuingia katika ndoa hii na Yanga ambayo ni klabu kongwe na wapenzi wengi hapa nchini, na tunawaomba watu wote wenye mapenzi na Yanga wajitokeze sasa na kuanza kuichangia klabu yao,”alisema Gallus.

Wakati huo huo Mkwasa amesema kwamba kikosi cha Yanga kitaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa mchezo mmoja wa kirafiki kikiwa njiani kuelekea Mwanza ambako Jumapili kitakuwa na mchezo wa mashindano.
Yanga watamenyana na Kombaini ya Majeshi Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma Jumatano, kabla ya Jumapili kuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sporrs Federation (ASFC).

Na mapema Jumatatu kikosi hicho kinatarajiwa kuendelea Dar es Salaam kuendelea na maandalizi ya mechi zake za viporo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
No comments: