Breaking News
recent

ENEWZ AFRICA | PICHA: HARMORAPA NDANI YA BONGO RECORDS KWA P-FUNK MAJANI



Iko wazi Harmorapa ametrend mtandaoni kwa mwezi mfululizo sasa, yani kwa publicity anayoipata ni kubwa sana. Harmorapa ameanza kufahamika baada ya kuibuka na kudai kuwa anafanana na Harmonize, na wengine wakaanzisha mzaha kuwa ni ndugu yake.
Na hata jina lake lina maana ya kuwa yeye ni Harmonize anayerap. Kwa muda mfupi watu wakaanza kumfuatilia na kwakuwa binadamu hupenda vitu kama hivi – mzaha, jina lake likasambaa haraka na focus ikahamia kwake, kuliko hata Harmonize mwenyewe.


Harmorapa
Hivi karibuni mtayarishaji huyo mkongwe alionyesha kupendezwa na harakati za rapper huyo ambaye amekuwa akizungumziwa kila kukicha na hiyo kupelekea Majani kumpost kwenye akaunti yake ya Instagram huku picha hiyo ikiwa na caption hii.. “Chezea @harmorappa wewe!!! Levo zingine hizi,” aliandika Majani kwenye picha hiyo na kuchomeka emoji ya kicheko. Hakuna ubishi, Harmorapa ametokea kuwa burudani kwa wengi.
Jumatatu hii alimtembelea producer mkongwe wa Bongo Record, P-Funk Majani nakuzungumza naye mambo kadhaa kuhusu muziki.
Rapper huyo baada ya kutembelea studio hapo na kukutana na mkongwe huyo alionyesha kufurahishwa huku akiwataka watu kuacha kuongea.


Dreams are brighter days!! Nikiwa na legend producer Majani. Ya leo siyo ya jana hatuongei ongei tu #shout out,” aliandika rapper huyo Instagram.
Kwa upande wa Majani alipost picha aliyopiga na rapper huyo na kuandika: “Harmorapa payed us a visit today”.

Hizi ni baadhi ya picha za Harmorapa & P Funk









No comments:


Powered by Blogger.