ENEWZ AFRICA | RAY C AWAGUSA WATANZANIA KWA KITENDO HIKI JUU YA MADAWA YA KULEVYA
Mkali wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama ‘Ray C’ Kiuno Bila Mfupa, amejitokeza kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda juu ya sakata zima la dawa za kulevya.
Kupitia video hiyo aliyoiweka kwenye akaunti yake ya Instagram, inamuonesha mtu aliyepoteza maisha kwa madawa ya kulevya huku akiandika: “SAY NO TO DRUGS”
Aidha Ray C ambaye anatajwa kama nimhanga wa madawa hayo aliwahi kupewa huduma vituo mbalimbali vinavyotoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya ‘Sober House’ na baada ya muda anaonekana kurudia hali ya kudhoofu na kuwa kama mhanga wa madawa hayo.
Kupitia video hiyo Instagram, Ray C amewahamasisha watu wengi na imeonesha kuwagusa Watanzania wengi kwa kuchangia maoni yao juu ya athari mbaya za madawa ya kulevya na sakata la linalonguruma kwa sasa nchini.
No comments: