‘Sitaki Ushambenga’ – Diamond
Kumtenganisha Diamond na Zari ni sawa na kutaka kutenganisha mchanga na mchele vilivyochanganywa pamoja, ni kitu ambacho kigumu na kitachukuwa miaka mingi.
Hitmaker huyo wa Marry You, ameonekana kuwacheka wabaya wake waliokuwa weakitokwa povu juu ya picha iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha Zari akiwa na kidume mwingine kwenye swimming pool.
Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameweka picha akiwa na malkia wake huiyo huku ukisikika wimbo wa TOT Modern Taarab ‘Sitaki Ushambenga’ na kuandika, “Nimesema staki ushambenga! @zarithebosslady .”
Jumatatu hii kupitia mtandao huo Diamond, aliweka picha ya mama watoto wake [Zari] akiwa kwenye swimming pool na kidume mwingine na kuandika maneno ambayo yalionekana kumuumiza.
Lakini baada ya muda mfupi Zari alijitetea kwa kuweka picha kadhaa akiwa katika eneo hilo na marafiki zake, mwanae Junior pamoja na jamaa huyo na kuandika, “Photo credit was by his wife. He is my kids’ uncle, the late’s cousin And I happened to meet them at a spa. When you are that IT loyal gal, someone will always find fault when it’s not there just to cover and turn around stories of all the dirty they do behind you back.”
Hata hivyo baadae Zari alizifuta picha hizo.
No comments: