Shaa aeleza sababu ya kufanya kolabo kiurahisi na chipukizi
Shaa afunguka sababu ya kukubali kufanya kazi na wasanii wachanga kiurahisi.
Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo Flava ambao hushirikina kwa ukaribu na wasanii chipukizi katika kufanya nao kazi bila hata ya kuwadai fedha.
Akiongea katika kipindi cha FNL cha EATV, Shaa amesema, yeye wakati anaanza muziki akiwa msanii mdogo aliweza kupata nafasi ya kumshirikisha AY kwenye wimbo wake ‘Pambazuka’ bila hata ya kudaiwa hela na msanii huyo, hilo ndio limempelekea kuvutika kufanya kitu kama hicho.
Baadhi ya nyimbo ambazo muimbaji huyo amefanya na wasanii hao chipukizi ni ‘Nikilewa’ wa Nasi kutoka Mbeya, na ‘Mali ya Mungu’ wa Biznea kutoka Mwanza na nyingine.
No comments: