Breaking News
recent

Nyoso apata shavu

Hatimaye aliyekuwa Nahodha wa Mbeya City, Juma Nyoso amepata kibarua kipya cha kusajiliwa na timu ya Kagera Sugar katika msimu mpya wa usajili uliofunguliwa leo rasmi.


Nyoso amesajiliwa na Kagera Sugar baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kumdhalilisha aliyekuwa Nahodha wa Azam FC, John Bocco ambaye kwa sasa amesajiliwa katika klabu ya  wekundu wa msimbazi, Simba.
Mbali na Nyoso Kagera Sugar pia wamefanikiwa kumsajili beki Japhary Kibaya kutoka Mtibwa Sugar, Viungo Peter Samson Mwalyanzi, Ludovic Venance na mshambuliaji Omary Daga maarufu kama ‘Dagashenko’ pamoja na kipa Hussein Kipao kutoka JKT Ruvu ambayo ilishuka daraja msimu ulioisha katika ligi kuu Tanzania Bara.

No comments:


Powered by Blogger.