Huddah Monroe ajisafisha kwa Zari
Unaukumbuka ule mtifuano wa Zari The Bosslady na Huddah Monroe uliotokea mwezi Julai mwaka jana? Huddah alidai kuwa Diamond ni mali ya umma, anaweza kugaiwa kwa mtu yoyote kama pizza na alishawahi kuwa naye kwenye mahusiano kipindi ambacho yupo na Zari.
Mrembo huyo wa Kenya amefunguka kuwa ule wote ulikuwa ni uongo wala hajawahi kuwa na mahusiano na bosi huyo wa WCB wakati tayari yupo na mahusiano na mama Tiffah.
“Reasons I don’t fu*k married men is coz I’m a feminist, I care about the next woman. Even allegation that I slept with Zari’s man when she was with him was all lies. But that’s what people are good at lying about me. To make me look like I’m BAD,” ameandika huddha kupitia mtanda wake wa Snapchat.
Vita hiyo ya maneno ilianza baada ya kudaiwa kuwa Zari amemkaushia Huddah kumpa mwaliko kwenye birthday party ya mtoto wake, Tiffah na mualiko huo kupewa hasimu wake Vera Sidika. Tazama snapchat zote hapo chini.
No comments: