Breaking News
recent

Simjui Beckham na hajawai kuwa mpenzi wangu – Iggy Azalea

Rapa wa kike, Iggy Azalea, mwenye asili ya Australia ambaye ameanza kuishi nchini Marekani tangu akiwa na miaka 16, ameibuka na kukana kutoka kimapenzi  na Odell Beckham ambaye ni mchezaji wa zamani wa American Football.


Kwa mujibu wa gazeti la Daily News lililotoka siku ya Jumatano, Iggy Azalea na Odell Beckham walionekana kuwa pamoja kwenye pati maeneo ya Bowlero Woodland Hills bowling yaliopo katikati mwa jiji la Los Anglese. Ukaribu huo umezusha uvumi kuwa huwenda wawili hao wakawa wanatoka kimapenzi.


Siku ya juzi mtandao wa TMZ ulimnasa Azalea na alitakiwa kutoa ufafanuzi juu ya mahusiano yake na Beckham.
“Simjui huyo Beckham.. sijawahi kuwa na mazungumzo naye” alisema Azalea huku akiwa anaficha macho yake kwa kuvaa miwani.
Picha hiyo ya Beckham Jr na Azalea ilipigwa May 15 wakiwa katika kundi na ikadaiwa wanamahusiano.

No comments:


Powered by Blogger.