MESSI ADAIWA KUGOMA KUSAINI MKATABA MPYA KISA HIKI
Mpango wa viongozi wa FC Barcelona wa kuhakikisha mshambuliaji kutoka nchini Argentina Lionel Messi anasaini mkataba mpya huenda ukaingia majaribuni, kufuatia mchezaji huyo kuhoji mambo kadhaa.
Kwa mujibu wa mtandao wa sportskeeda.com umeeleza kuwa, Messi ametaka uongozi wa Barca kumueleza mustakabali wa meneja wao wa sasa Luis Enrique, na kama ataondolewa ni nani atakaepewa nafasi yake, pia ametaka aambiwe wachezaji ambao wataingai kwenye soko la kuuzwa na wale watakaosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Messi amehoji mambo hayo na kutaka apatiwe majibu haraka iwezekanavyo, ili aweze kufanya maamuzi ya mwisho ya kusaini mkataba mpya ama kuendelea na mkataba wa sasa ambao utafikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao.
Messi amesisitia majibu wa masuala hayo, kwa kutaka kujiridhisha kama kweli ataendelea kuwa na furaha endapo ataamua kubaki klabuni hapo kwa kipindi kingine kirefu. Tayari taarifa zinasema, endapo Messi atashindwa kupatia majibu ya masuala hayo kwa muda anaoutarajia, huenda akafanya maamuzi ya kuelekea nchini China mwishoni mwa msimu ujao.
Wakati hayo yakitokea bado uongozi wa Barca umeendelea kusisitiza suala la mkataba mpya wa Lionel Messi litakamilishwa kwa maelewano ambayo pande zote zitayaafiki.
No comments: