Kocha wa Uingereza achekelea mfumo mpya timu ya taifa
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate, amesema ”amefurahishwa sana” na jinsi upande wake ulivyokumbatia mfumo mpya wa mchezo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani
Mshambuliaji Lukas Podolski alipiga kombora safi kutoka mbali na kuipata ushindi Ujerumani 1-0 huko Dortmund.
Southgate amesema aliamua England itacheza kutumia mfumo wa 3-4-3 ”karibu wiki sita zilizopita”.
Alitumia mabeki watatu kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwao na Croatia mwaka 2006.
Tunastahili kutafakari zaidi kwa matokea bora, Southgate aliambia BBC Radio 5.
Kufuatia mchezo wake wa kwanza kama meneja wa England, 46, aliongezea: ”Kwa mechi hizi ni muhimu kujifunza kitu kutoka kwa mchezo, na muhimu zaidi ni kiwango cha mchezo kuwa juu.”
”Ilikuwa jambo jema kujiweka katika kiwango cha juu kwao, ndio tuweze kuwa na nafasi za kukabiliana nao katika mashambulizi, jambo ambalo lingewasababishia shida, na hivyo ndivyo ilivyokuwa.”
Hatahivyo, Southgate amesema alikuwa na kikosi ambacho kina uwezo wa kucheza ”mifumo tofauti.”
”Tulikuwa tishio kwa wapinzani wetu katika eneo la mashambulizi, na tuliweza kupenya katikati yao pia,” aliongeza.
”Tuna wachezaji tofauti. Iwapo unataka kucheza na washambuliaji, basi wana uwezo wa kucheza katika nafasi yoyote. Tumeona uwezo na udhaifu wa wapizani wetu.”
Source: BBC
No comments: