Breaking News
recent

HHII NDIO SABABU YA KUTOUONA UKARIBU WA ALIKIBA NA BARAKA DA PRINCE KWASASA


Baraka Da Prince ni msanii ambaye alikuwa akionekana kuwa karibu sana na msanii mwenzake Alikiba siku zilizopita. Ikiwa ukaribu wao ulikuwa ni wa kikazi na hata ushkaji wa kawaida.
Ni ukweli usiofichika kwamba wawili hao hivi sasa hawana ukaribu kama waliokuwa nao hapo awali. Kutokana na kutoonekana pamoja kama zamani na vitu kama hivyo.
Maswali yamekuja katika vichwa vya wengi kuhusu wawili hao, huenda wamegombana au kuna kipi kinachoendelea kati yao.
DJ PAUL24 imeamua kupiga story na meneja wao katika lebo ya Rockstar4000 Seven Mosha ili aweze kutuambia kunani baina ya wawili hao.
“Hamna distance baina ya Baraka na Alikiba, katika lebo yetu kila msanii anajitegemea, Baraka hivi sasa  yuko katika harakati za kumaliza album yake, pia ana shows zake ambazo anapiga ndio maana hamuoni ukaribu.” ALisema Seven Mosha.

No comments:


Powered by Blogger.