Breaking News
recent

UDAKU | BABU TALE AFUNGUKA JUU YA KUFANANA KWA VIDEO NYINGI ZA MUZIKI WA BONGO FLEVA


Babutale ni meneja maarufu wa kundi la bongofleva la Tip Top connection lakini pia ni meneja wa mwimbaji Diamond Platnumz ambapo leo Tale ameguswa na baadhi ya video kadhaa za bongofleva kufanana.
Hili limekuja baada ya kuzitazama video hizo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tale ameandika haya…

Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Hii ni kwa ndugu zetu madirector wa nyumbani tanzania, tunaomba angalau muwe mnajishugulisha kuangalia vitu ambavyo havijatumika ili kuepuka kufananisha video zetu,sababu inapelekea wasanii kukimbia na kwenda kufanya kazi zao nje ya nchi.
Aliongeza, Mfano kuna video ya dogo janja na roma zote location moja,madee bilnas na wengine wote wametumia vitoa moshi,chege na ben paul wote wametumia gari moja,hilikosa ni la msanii au director? #kelele_za_chura@chegechigunda
Kwa upande mwingine tukiangalia suala hilo la kufanana kwa video nyingi za muziki wa Bongo Fleva inatokana na mawazo ya wasanii wenyewe.
Mara nyingi Ukiona kuna kitu kimerudiwa katika video ujue kuna makubaliano kati ya muongozaji na msanii kwakuwa mara nyingi msanii anapoandika wimbo wake anakuwa na wazo la aina ya video ambayo anaitaka hivyo wasanii ni kama wateja kwa ma-director.



No comments:


Powered by Blogger.