SPORTS EXTRA | Yanga ya toa kichapo kwa wa Comoro
Mabingwa wa Tanzania bara Dar es Salaam Yanga Africans wamecheza mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza wa Club Bingwa barani Afrika ugenini dhidi ya N’gaya Club ya Comoro Jumapili ya February 12.
Yanga wameanza vizuri mawindo yao ya ubingwa wa Afrika, baada ya kuwachapa wenyeji Ngaya Club de Mde mabao 5-1, mjini Moroni, Comoro.
Ushindi huo unamaanisha Yanga watakuwa na shughuli nyepesi tu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Dar es Salaam, kwani hata wakifungwa 3-0 watasonga mbele.
Kiungo Mzambia, Justin Zulu alifungua akaunti yake ya mabao Jangwani baada ya kusajiliwa msimu huu kwa kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 43.
Winga machachari, Simon Happygod Msuva akaifungia Yanga bao la pili dakika ya 45 na Yanga ikaenda kupumzika inaongoza kwa mabao 2-0.
Mzambia mwingine, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya 59, kabla ya Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe kufunga la nne dakika ya 65 na Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tabo dakika ya 73.
Ngaya walijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 66 kupitia kwa Said Anfane Bourah Mohammed aliyetokea benchi kipindi cha pili.
No comments: