ENEWZ AFRICA | Picha: Manji aonekana akitolewa polisi na gari la wagonjwa
Mfanyabiashara Yusuf Manji Jumapili hii alionekana akitolewa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi na kupandishwa kwenye gari la wagonjwa ambalo lilipita Barabara ya Sokoine kuelekea Posta Mpya.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Manji akipanda gari hilo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lakini hawakufahamu mara moja alikoelekea.
Manji alikuwa amevaa fulana, suruali na viatu vya wazi vyote vya rangi nyeusi
Mwenyekiti huyo wa Yanga anashikiliwa na jeshi hilo kwajili ya mahojiano kuhusu tuhuma zinazomkabili za kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya.
No comments: