Breaking News
recent

ENEWZ MAMTONI | Kanye West ajiondoa kumuunga mkono Trump

Kanye West ana mabadiliko ya hisia zake za moyoni. Unakumbuka aliwahi kusema kuwa kama angepiga kura angemchagua Donald Trump? Alienda mbali zaidi na kukutana na Rais huyo New York.



Na sasa Yeezy amerudisha kadi yake, hamuungi tena mkono. Kwa mujibu wa TMZ, Kanye ameziondoa tweets zote alizoandika kumfagilia Trump.
Mtandao huo umesema rapper huyo amechukizwa na sera za kibaguzi za rais huyo wa 45 ikiwemo ya kuwazuia waislamu kuingia Marekani.
Kanye alikuwa mmoja wa wasanii wakubwa wachache waliokuwa upande wa Trump. Hata mkewe Kim Kardashian, ni mmoja wa mastaa wanaompinga vikali rais huyo.
Mwezi uliopita rapper T.I. alimuita Kanye msaliti.

No comments:


Powered by Blogger.