Breaking News
recent

ENEWZ MAMTONI | ibu kubwa kwa Dj Khaled na Jay Z…..



Wasasema ni kawaida kwa wasanii kukutana na changamoto kama hizi za kuambiwa umeiba kazi ya mtu ila kwa kesi ya DJ Khaled inasemekana ni kweli jambo hili kalifanya.
Chris Hill amejitokeza na kudai chake baada ya kusikia kazi ya mikono yake ikitumika kwenye wimbo wa “I Got the Keys” wa Dj Khaled aliosikika Jay Z , Future na wasanii wengine.
Producer Chris Hill anasema mdundo uliotumika kwenye wimbo huo ulikuwepo kwenye cd aliyompya Dj khaled March 2008, cd hii ilikuwa “Chris Hill Beats (Gangsta Boogie Vol 2)“.

Chris anasema alikutana na Khaled October 2008 mjini Atlanta na kumpa Cd hio na miaka nane baadae anaisikia kazi yake kwenye wimbo na wasanii kama Jay Z bila ruhusa yake wala malipo yoyote.
Kutokana na mafanikio makubwa ya wimbo wa “I Got the Keys” wenye watazamaji milioni 79 YouTube Producer Chris amefungua kesi ya madai dhidi ya Dj Khaled, Sony Music na Producers waliofaidika na wimbo huo.

No comments:


Powered by Blogger.