ENEWZ MAMTONI | Documentary mpya ya maisha ya Nototrious B.I.G. imeanza kuandaliwa…
Kampuni ya Submarine Entertainment na ByStorm Film wameanza kutayarisha Notorious B.I.G.: One More Chance, Filamu hii fupi itatayarishwa na Emmett na Brendan Malloy,mama yake B.I.G ‘Voletta Wallace’ atahusika.
Mama yake B.I.G alisema kwenye taarifa kwa vyombo vya habari kuwa anafuraha kuona muziki na maisiha ya mtoto wake bado yana nafasi kubwa kwenye muziki na maisha ya vijana wa sasa.
Submarine wamewahi kushika dili kubwa za maisha ya mastaa kama Nas: Time Is Illmatic na Searching for Sugarman.
Hijatajwa inatoka lini filamu hii ya One More Chance, ikiwa mwaka huu tunatimiza miaka 20 toka kifo cha B.I.G.
No comments: