Breaking News
recent

BEEF | “Unatoa wapi vigezo vya kumuwakia Profesa Jay?” – MwanaFA



MwanaHipHop kutoka Tanzania Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA hajapendezwa na ishu iliyotrend kwenye mitandao hivi karibuni ya kumkosoa Mkongwe wa Hiphop Tanzania Profesa Jay ambapo ishu ilianzia kwenye swali la msanii wa Hiphop Nash MC.
Baada ya swali la Nash MC, Profesa Jay aliandika kwenye Twitter page yake >>> “Juzi tu dogo @NashEmcee aliuliza hivi Singeli imeshakwenda International? nilitegemea angeuliza kwanini HIPHOP ya Bongo haivuki boarder? badala wa kujiuliza tumekosea wapi sasa tunakua na wivu wa kijinga na kuchukia mafanikio ya wengine waliopambana kufika hapo walipo sasa”
Baada ya Tweets kadhaa za Profesa Jay Nash Emcee alijibu kwenye Twitter pia kwa kuandika Tweets kadhaa >>> “Nna uhuru wa Kuongea nachotaka almuhimu nisivunje sheria za nchi,hakuna pimbi yoyote anaweza kunipangia swali la kuuliza kwenye muziki, nidhamu ya uoga kwangu ilikaaga upande wa kushoto kitaaaaambo”
Baada ya hii kuendelea kusambaa mitandaoni, MwanaFA akachukua time yake kwenye Twitter na kuandika kwa kuanza na kuzitaja HITS za Profesa Jay >>> “Chemsha Bongo,Bongo DSM,Jina Langu,Nikusaidiaje,Zali La Mentali,Promota Anabeep,Ndio Mzee,Hapo Vipi,Msinitenge, Niamini… mpaka nyingine nashindwa kukumbuka haraka”
Come on man, hakuna mtu kwenye mziki wetu ana sifa za kumkosoa huyu ‘mzee’ tena kwa kumkosea adabu, sijui kwa nini wakati mwingine tunafanya tunayofanya, I guess ndio ‘ushujaa’ wenyewe huo lakini ukiwa kwenye utimamu kabisa wa akili, HUTHUBUTU
Unatoa wapi vigezo vya kumuwakia mtu aliyeubadili mziki PEKE YAKE ukafikia kusikilizwa na rika zote nchi nzima? uliufanyia nini mziki cha kukupa wadhifa huo? come on, najua kuwa ‘muasi’ ni ‘sifa’ ya hiphop lkn tafadhalini muwe na viwango aisee, vinginevyo,love and respect tu..sina zaidi aisee

No comments:


Powered by Blogger.