UDAKU | KHADIJA YUSUF ATAJA SABABU HII YA JAHAZI KUVUNJIKA
Hapo siku za nyuma msanii wa kundi la Jahazi Amigo, aliwahi kusikika akisema baada ya Mzee kuacha muziki wasanii walianza kuyumba kiuchumi na baadhi ya wasanii kuona maisha yao yatakuwa magumu na kuanza kuhama mpaka sasa wamebaki wasanii 4 kwenye bendi ya Jahazi.
Pia Amigo alisema bendi ya Jahazi ilikuwa chini ya Hamisi Doa baada ya Mzee kuondoka lakini pia hata Khadija Yusuf alipewa kipaumbele cha kutosha na alikuwa akishirikishwa katika vitu vingi katika bendi hiyo anashangaa ni kwa nini aliamua kuondoka na kuwaacha.
Sasa basi, Msanii wa taarabu nchini Khadija Yusuf amejibu shutuma hizo kwa kusema hakuna tena kundi la Jahazi Morden Taarabu kwa sasa na tayari wamegawana vitu vilivyokuwa ndani ya kundi hilo na yeye kwa sasa yupo kwa Thabit Abdul.
Khadija Yusuf
Akiongea ndani ya eNews Khadija amesema Jahazi limevunjwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa Mzee Yusuf wakati anaacha muziki alisema hata vunja kundi hilo lakini Mungu mwenyewe ndo atalivyunja na tayari dua yake imepokelewa na Mungu.
Pia Khadija amesema kwa sasa furaha ya kaka yake Mzee Yusuf imekamilika kwa sasa na dua zake pia zitakuwa zime pokelewa na Mungu kama alivyokuwa akiomba kwamba ifikie kipindi hata nyimbo zake zisiwe zinapigwa.
No comments: