Breaking News
recent

UDAKU | MKONGO AMVURUGA KADJANITO, ABADILI NA DINI, AFUNGUKA KUHUSU KUOLEWA



Msanii wa Bongo fleva Khadija Said Maige
maarufu kama Kadjanito amefunguka na kusema kuwa amepagawa na mapenzi ya Tresor Lisimo mchezaji wa mpira ambaye ndiye anataka kufunga naye ndoa tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka huu.
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZAO




Kadjanito kupitia kipindi cha eNewz anasema aliona amekaa peke yake kwa muda mrefu hivyo ameamua kuwa mke wa mtu ili na yeye awe mwanamke aliyekamilika sababu amempata mtu anayependana naye na mtu ambaye wanaelewana.
“Nimeamua kufunga ndoa kwani nilikaa muda mrefu peke yangu nikatafakari nikaona siyo kitu kizuri nikiwa kama msichana ambaye nina ‘Inspire’ watu wengi lazima kuna vitu nifanye ili niwe mwanamke kamili, maana ukiwa peke yako mtu anaweza kukuchukulia labda huyu mtu muhuni lakini mimi nimeamua kuwa mke wa mtu, najua ni kitu kikubwa lakini haitanifanya mimi niache kazi zangu za muziki”
Ameendelea kusema “Nimeamua kufunga ndoa sababu nimeona nimepata mtu ambaye tunapendana, ninaendana naye na ninampenda sana. Aisee mimi nafunga ndoa ya Kikristu yaani jamaa nimemzimia mpaka nimeamua kumfuata katika imani yake, kiukweli ninamfuata” alisema
Kadjanito

No comments:


Powered by Blogger.