UDAKU | Makinda ahofia kuongezeka kwa matumizi ya madawa ya kulevya nchini
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, amesema jitihada za kupambana na dawa za kulevya zinatakiwa ziongezwe kwa kuwa zinawaathiri wanafunzi wa shule za sekondari nchini.
Makinda aliyasema hayo Jumapili hii wilayani Same, Kilimanjaro alipokuwa akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mtakatifu St.Joachim.
“Matumizi ya dawa za kulevya katika shule za sekondari yamekuwa ya kawaida ingawa madhara yake ni makubwa katika jamii. Madawa hayo yanachangia maadili kumomonyoka kwani kuna baadhi ya vijana wa kiume wanalawitiana wenyewe kwa wenyewe,”alisema Makinda.
“Hali kwa sasa si nzuri, yaani matumizi ya dawa hizo yameongezeka, ndiyo maana ninasema kuna haja ya kuongeza nguvu za kupambana na matumizi ya dawa hizo,” aliongeza.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments: