Breaking News
recent

Pam D: Sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mesen Selekta

Pam D amekanusha kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na producer wake, Mesen Selekta


Ameiambia Bongo5 kuwa, yeye ni first lady wa label ya Mesen, Team Selekta na kwamba uhusiano wao ni wa kikazi tu.
“Watanzania wamezoea kwamba mara nyingi wakimuona mtu anaimba na mtu halafu nyimbo imefanya vizuri, wanaamini ‘ahh lazima watakuwa wapenzi.’ Kwahiyo hawajui kwamba watu wanaweza wakafanya kazi kama ndugu na zikafanya vizuri,” amesema.
“Kwahiyo mimi na Mesen ni ndugu, yule yeyote anayeamini sijui ni wapenzi wafute hivyo kwasababu hata wakikaa kwenye Insta ukisoma ‘wewe usifanye hivyo unajua Mesen anakuona.'” ameongeza.
Pam amedai kuwa kazi zake nyingi ataendelea kuzifanya chini ya Mesen. Hivi karibuni aliachia video ya wimbo wake mpya, Daffa.

No comments:


Powered by Blogger.