Breaking News
recent

DESIIGNER, TORY LANEZ, YOUNG M.A NDANI YA LISTI YA FORBES


Ukiachana na wasanii wakubwa ambao wanaongoza listi ya wasanii wa HipHop wanaoingiza mkwanja mrefu wakiwemo kama Diddy, Jay Z na Dr. Dre, Forbes wamekuja na listi nyingine ya FORBES HIP-HOP CASH PRINCES 2017.
Ndani ya Listi hiyo unakutana wasanii wakali ambao wanachipukia katika game hii ya muziki na wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafanya vizuri na kuteka soko kubwa la mashabiki katika tasnia yao ya muziki.
Ukiachana na listi iliyopita ambayo iliwashirikisha Boi-1da, DeJ Loaf, Fetty Wap, G-Eazy, Joey Bada$$, Lil Dicky, Logic, na Metro Boomin, hii ndio listi mpya ya waliopewa cheo hiko na jarida hilo la Forbes.
FORBES HIP-HOP CASH PRINCES 2017
Desiigner
D.R.A.M.
Tory Lanez
Lil Uzi Vert
Lil Yachty
Noname
Isaiah Rashad
Stormzy
Bryson Tiller
Young M.A.

No comments:


Powered by Blogger.