Breaking News
recent

Hanscana adai video ya ‘Kidebe’ ya Dogo Janja iliwaingiza chaka

Kumbe video ya ‘Kidebe’ iliwaingiza chaka Hanscana na Dogo Janja!


Hanscana amekiambia kipindi cha On The Eight cha ETV kuwa nyumba waliotumia kushoot video hiyo waliipata kiujanja ujanja na walipomaliza kushoot wakagundua kuwa mwenyewe ni mtu mkubwa jeshini.
“Wakati tunatafuta nyumba ya kushoot mimi na Dogo Janja tukaiona ile nyumba tukaingia, tulikutana na house girl ambaye hajui hata neno kushoot. Tulimwambia baba katutuma akaturuhusu tukaanza kushoot lakini wakati tunamaliza tukasikia honi kumuona mwenyewe ana vyeo kibao, ni mtu mkubwa huko jeshini. Tukaanza kumuomba msamaha sana mwisho alituambia ondokeni,” amesema Hanscana.
Muongozaji huyo wa video hapa nchini ameongeza kuwa kwa mwaka huu alikuwa na mipango ya kushoot video 12 na tayari ameshashoot video saba na zilizobaki tayari ameshakuwa booked.

No comments:


Powered by Blogger.