Breaking News
recent

Mshambuliaji wa Zanako Aionya Yanga


Mshambuliaji hatari wa Zanaco, Fashion
Sakala jana alituma salamu kwa Yanga baada
ya kuifungia mabao mawili timu ya taifa ya
Zambia ya vijana wenye umri chini ya miaka
20 katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Mali
kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini
ya miaka 20.
Sakala maarufu kwa jina lake la kwanza la
Fashion alifunga mabao hayo mawili dakika ya
8 na 66 na kumfanya kuwa nyuma ya kinara
Luther Singh wa Afrika Kusini mwenye mabao
matatu.
Akiwa na umri wa miaka 19 tu tayari
anatatajwa kuwa mmoja wa washambuliaji
watakaojenga kikosi kipya cha Zambia.
Alikuwa msaada mkubwa kwa Zanaco kuivua
taji la Ligi Kuu Zambia klabu ya Zesco United
kwa kufunga mabao kumi msimu uliopita.
Ni mfungaji bora wa michuano ya COSAFA
U-20 iliyopita huku akiwa ameshamwaga wino
katika klabu ya Spartak Moscow ya Urussi.
Hata hivyo kuna uwezekano mdogo sana wa
kucheza pambano la awali dhidi ya Yanga
kwani mechi za mshindi wa tatu na fainali za
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
zitachezwa wikiendi moja na mechi za awali
za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa
Afrika.
Kwa hesabu hizo, Fashion ambaye ni dhahiri
amedhihirisha kuwa ni mmoja kati ya
wachezaji wanaotakiwa kuchungwa na Yanga
anaweza kucheza pambano la marudiano
litalopigwa huko Zambia kati ya tarehe 17-19
Machi.

No comments:


Powered by Blogger.