MAMBO MAKUBWA MATATU YANAYOSUBIRIWA KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ
Hii ni baadhi ya miradi ambayo msanii wa Bongo Fleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz alitangaza kuifanya na sasa mashabiki wake wanaisubiria kwa hamu kubwa.
1. Wasafi Tower
Jengo hili Diamond alieleza kuwa lipo maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam na litakuwa na Ofisi na Hoteli, pia lebo ya WCB Wasafi na biashara zake nyingine zitahamia hapo.
Kufika Oktoba mwaka jana Diamond alitumia ukurasa wake Twitter kutaarifu umma kuwa ujenzi wa Wasafi Tower umefikia asilimia 95, hivyo muda wowote watu wataona jengo hilo. Hilo bado linangojewa!.
2. The Real Life of Wasafi
Juni 19, 2018 Diamond alitangaza kuanza kwa kipindi cha Televisheni kitakachokuwa kinaonyesha maisha ya watu wote wanaohusika na WCB Wasafi na bidhaa zake. Hilo bado linangojewa!.
"Tungependa kuwatangaza rasmi kwamba Ijumaa hii ile TV Show yetu ya The Real Life of Wasafi inakuwa rasmi kuanza, kwa hiyo waliyoko nyumbani tutawaambia itaanza kuruka saa ngapi" alisema Diamond wakati akiongea na Wanahabari, Dar es Salaam.
3. Wasafi Betting
Baada ya kuwa Balozi wa moja ya kampuni ya michezo ya kubashiri, naye Diamond alitangaza kuwa yupo mbioni kufungua ya kwake maana aliona ni biashara nzuri. Hilo nalo, bado linangojewa!.
"Nipo hatua za mwisho, hivi karibuni nafungua Wasafi Betting" alisema Diamond Oktoba mwaka jana wakati akiongea na kipindi cha The Switch cha Wasafi FM.
No comments: