SHETTA AELEZEA NIA YA KUTANGAZA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA
Wiki mbili zilizopita kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii wa Bongo fleva Shetta alitangaza kuwa katika msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani anatarajia kutoa misaada katika vituo vya kulelea watoto yatima katika mikoa mbali mbali nchi nzima.
Kitu ambacho kilileta mtazamo tofauti kwa baadhi ya watu na kudai kwamba sio vyema kutangaza kwa watu kama unania ya kutoa msaada.
DJ PAUL24 imemkamata Shetta kwenye exclusive interview na ameweza kulizungumzia jambo hilo ikiwa ni pamoja na sababu za yeye kutangaza kufanya jambo hilo.
“Katika dini me naamini hautakiwi kutangaza, kutangaza kwangu mimi na management yangu ni kwamba kuna sehemu hatuvijui vituo na tunataka tuwafikie kirahisi ndio maana tukaamua kutangaza,” Alisema Shetta
No comments: