Breaking News
recent

Vanessa Mdee ampata mrithi wa Jux ? aonekana akila bata na msanii huyu wa Marekani

Msanii na  mrembo kutoka nchini Tanzania Vanessa Mdee huenda akawa katika penzi jipya na msanii mwenye asili ya Nigeria anayefanya shughuli zake Marekani aitwaye Rotimi.


Wawili hao wameoneakana wakiwa pamoja  katika sehemu ya mapumziko kwenye bwawa la kuogelea “swimming pool” huko nchini Marekani huku wakila bata na kuvinjari.
Aidha kama haitoshi wawili hao walirekodi video fupi ikionyesha wakiwa pamoja kupitia Insta Story ya mtandao wa kijamii wa Instagram na  hata picha za mwisho walizopost kupitia mtandao huo mahali “Location” ilisoma wakiwa sehemu moja.

Pia kupitia post hizo hizo za Insta Story za mtandao huo wa Instagram Vanessa Mdee alitangaza kuwa sasa hivi atakuwa ana “block”sana watu kupitia mitandao ya kijamii.
Vanessa Mdee alikuwa na mahusiano na msanii wa RnB Bongo Juma Jux kwa muda wa miaka 6, ila walitoa taarifa za kuachana kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya mahojiano  kwenye vyombo vya habari mwezi wa 7 mwaka huu.

No comments:


Powered by Blogger.