Breaking News
recent

Vanessa Mdee amtoa povu Baby Madaha

Msanii wa muziki wa Bongo Flava Baby Madaha ameonekana kuumizwa na Vanessa Mdee kutajwa mara kwa mara mwenyewe kuwania tuzo za muziki za nje.


Akiongea na watangazaji wa Sibuka FM katika kipindi cha 180 Power, Byno na Joco, Baby japo hakulitaja jina la Vanessa lakini kutokana na maelezo yake ameonekana kuumgusa muimbaji huyo na kumtaja kuwa hana vigezo vya kutajwa katika tuzo hizo.
“Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo,” amesema Madaha.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa sasa ni wakati wa wasanii kuacha kuwa na uteam kwani muziki wetu unahitaji ushindani na tusupport.

No comments:


Powered by Blogger.