Breaking News
recent

Uganda: Mahakama yatoa amri kufukuliwa kaburi la Ivan

Zimepita siku tatu toka aliyekuwa mfanyabiashara maarufu Uganda, Ivan Ssemwanga kuzikwa huku moja ya matukio makubwa katika msiba huo likiwa ni kundi la Rich Gang kumwaga fedha kwenye kaburi, Ijumaa hii Mahakama ya nchi hiyo imetoa amri ya kuitaka Bank ya Uganga kufukua kaburi na kuchukua pesa hizo.


Kaburi la Ivan ndani likuwa na hela
Taarifa na Mahakama ya nchi hiyo inasema “The purposes of the said monies put into the grave were misused and there was wastage of public property thereby violating social and economic rights of other people,”
Pia Mahakama imeiamuru Benki Kuu ya Uganda kufukua kaburi na kuziondoa pesa hizo.
Kwa upande wa Benki Kuu ya Uganda imetoa tamko la kutaka vyombo vya dola viwachukulie hatua waliotupa hela kwenye kaburi la Ivan Don wakati anazikwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya wanasheria wakiongozwa na Tugume Gideon wa Human Rights Defenders Association Uganda kudai hawakufurahishwa na kitendo cha Rich Gang cha kuzika mamilioni ya pesa ndani ya kaburi, na kumua kwenda Mahakamani kuomba kaburi la Ivan lifukuliwe pesa zitolewe zikafanye shughuli nyingine na waliohusika washitakiwe kwa kuharibu kwa makusudi alama ya taifa.
Hii ni taarifa kamili ya Mahakama…


No comments:


Powered by Blogger.