Breaking News
recent

Urembo ni zaidi ya sura na umbo – Miss Tanzania 2016

Miss Tanzania namba mbili mwaka 2016, Maria Peter amesema watu wabadilike kimtazamo kuhusu shindano la Miss Tanzania kwani shindano hilo ni zaidi ya uzuri wa sura na umbo.


Mshindi wa Miss Tanzania, 2016 Diana Edward (katikati) akiwana msindi wa pili, Maria Peter na wa tatu Grace Malikita.
Mrembo huyo amesema mara baada ya kumalizika kwa shindono la mwaka jana ambapo Diana Edward alishinda, watu wengi walikuwa wakikosea bila kujua vigezo vingine vinavyoangaliwa nje ya uzuri wa sura katika mashindano hayo ya urembo.
“Ningependa kuwa elimisha, mashindano ya urembo ni zadi ya kuwa na uzuri wa sura, ni zaidi ya msichana kuwa na mvuto. Vipo vitu vingi sana ambavyo majaji walikuwa wanaangalia na kuwapa watu ushindi. Na basically Miss Tanzania ina lengo la ku-bring confidence kwa wasichana wa Tanzania,” Maria amekiambia kipindi cha E Newz cha EATV.
“Kwa hiyo tunaangalia mtu ambaye ataenda kuwakilisha Tanzania nje lakini sometime watu wanafikiria Miss Tanzania awe mzuri kama malaika vile, Miss Tanzania ni zaidi ya pale. Nashauri yanapotokea mashindano watu waache kuangalia muonekano wa nje, mtu anaweza kuwa na muonekano wa nje lakini she is not potential,” ameongeza.

No comments:


Powered by Blogger.