Breaking News
recent

Nikki Mbishi amjibu Godzilla kwa kebehi, ‘anaishi maisha ya kuigiza’

Baada ya rapper Godzilla kumuita Nikki Mbishi ‘wack’. Nikki amefunguka na kusema Godzilla anaishi maisha ya kuingiza na anaumia baada ya kushuka kimuziki mapema kitu ambacho hakukitarajia.


Nikki ameeleza kuwa akisema amzungumzie Godzilla kwa sasa hivi anabaki kumuhurumia kwani ameshapagawa na hajui afanye nini hasa pale anapoona uwekezaji ulioufanya unamnufauisha mtu mwingine.
“Ukiniita mimi wack kwa maana ipi, labda sijui kuandika, au wack kama yeye hajui anachokifanya anaishi maisha ya kuigiza, kujifanya wewe unaisha maisha ya Ulaya wakati upo Salasala unadanganya watu kuna all stars zimeninginizwa kwenye nyaya za umeme whichi is not true. Ana stress zake kaenda kwenye ufalme ambao sio wake sasa karudi huku ambako pengine akitakiwa awepo amekuta walfalme ni wengine sio yeye tena,” amesema Nikki.
Nikki amesema anafurahi jinsi Godzilla anamtaja kila mara katika interview zake kwani bila kufanya hivyo interview yake haiwi kali, na suala lake sio kupanda na kushika katika muziki bali ameshushwa na waliompandisha bila yeye kutarajia hilo.
“Zizi ametupwa halafu ameenda kuporomokea sehemu ambayo hata hajui atanyanyukaje, halafu ana watu wake anahitaji kuwasema ila anaona Nikki mwanangu nikiongea nitammudu fresh, kwanini awe muoga mbona mimi nawaambiaga,” Nikki ameikiambia kipindi cha Planet Bongo.
Nikki ameongeza kitendo cha Godzilla kuamni ujio wa Bill Nass kwenye muziki umemuondosha kwenye nafasi yake ndicho kinamdhohofisha na kumuua kimuziki.
“Ukisema fulani alikuja akafanya kama wewe ndio ukufa ina maana hata wewe ulikuwa hauna option, yaani maisha yako yanatengemea kitu kimoja kwamba hicho kitu kikishindikana na wewe umefeli, kwa hiyo unataka kuniambia Bill Nass alikuwa amepangiwa asifanye muziki kwa sababu atamuharibia Zilla soko lake, sio kweli,” ameeleza Nikki Mbishi.

No comments:


Powered by Blogger.