Breaking News
recent

Huu ni mwezi wa toba, mambo yote nimeyapiga chini – Harmorapa

Msanii wa muziki wa hip hop, Harmorapa amefunguka kwa kudai kuwa katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani kuna vitu vingi amekatazwa na menejimenti yake kuvifanya.


Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nundu’ , ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa amekatazwa kabisa kufanya interview au kwenda kwenye media kwaajili ya mahojiano.
“Kusema kweli kila mtu anajua huu ni mwezi mtukufu hata uongozi wangu wenyewe uliniambia nisifanye inteviews. Kwa hiyo nachoweza kusema ni kwamba mwezi huu kuna vitu vingi nimevipunguza, hata ishu ya interview labda kuwe na dharura au nipigiwe simu naweza kuzungumza lakini siyo ishu za huyu kasema hiki, huyu kasema kile,”
Rapa huyo ambaye anadaiwa kufanya muziki wake kwa kutegemea kiki, amesema kiki nyingi huwa zinamfuata na sio kwamba anazitengeza.

No comments:


Powered by Blogger.