DIAMOND PLATNUMZ AOMBA MSAMAHA KWA ASKOFU GWAJIMA! KISA WIMBO WA “ACHA NIKAE KIMYA”
Usiku wa kuamkia leo April 8 msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz aliachia ngoma ambayo ameipachika jina la Acha Nikae Kimya, ngoma flani hivi ambayo amezungumzia matukio yanayotokea nchini kwasasa.
Mmoja kati ya mistari ya Diamond Platnumz katika wimbo huo ulikuwa ukimuhusisha kiongozi wa kanisa la Ufufuo na uzima Askofu Josephat Gwajima na ulikuwa ukisomeka kama “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…”
Askofu Gwajima aliupokea tofauti mstari huo na kuandika ujumbe mzito kumuhusu Diamond Platnumz kwa kitendo hicho cha kimtaja kwenye wimb ohuo ambao alidai kwamba una lengo la kupotosha haki na kusapoti vyeti feki.
Diamond Platnumz baada tu ya kufikiwa na ujumbe huo hakuona aibu na kutumia kurasa yake ya instagram na kuandika maneno mazito ya kuomba radhi na kujaribu kumuelewesha Askofu huyo maana yake ya kumtaja katika wimbo wake huo.
Caption ya Diamond ilisomeka kama “Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…”
Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi?
Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho , mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima,” aliandika Diamond Instagram.
No comments: