REAL MADRID MBIONI KUFANYA MCHUJO HUU
Rais wa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid Florentino Perez, amekamilisha mpango wa kupata orodha ya walinda mlango ambao wataingia kwenye mchakato wa kusaka nafasi ya kusajiliwa klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa sportv4.com imedai kuwa Perez tayari ameshatangaza mlinda mlango wa sasa wa Real Madrid Keylor Navas ataondoka mwishoni mwa msimu huu, na nafasi yake itajazwa na mlinda mlango ambaye atakua na kiwango cha hali ya juu.
Orodha ya walinda mlango ambayo ipo mezani mwa rais huyo lipo jina la David de Gea wa Manchester United, Thibaut Courtois wa Chelsea, Bernd Leno wa Bayer Leverkusen, Hugo Lloris wa Tottenham na Gianluigi Donnarumma wa AC Milan.
Mmoja kati ya walinda milango hao atasajiliwa na kuwa chaguo la kwanza la Zinedine Zidane kuanzia msimu ujao wa ligi ya Hispania.
Hata hivyo mlinda mlango wa Spurs Hugo Lloris, anatajwa kuongoza kwenye orodha hiyo, kutokana na kumridhisha rais wa Real Madrid kwa kuwa na kiwango kizuri.
Lakini sababu hiyo haitokua kigezo kwa Lloris kusajiliwa moja kwa moja na magwiji hao wa mjini Madrid, bali walinda mlango wote walio kwenye orodha hiyo watapita kwenye mchakato ambao utakua chini ya mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo.
Real Madrid wamekua katika wakati mgumu wa kupata mlinda mlango mahiri, tangu alipoondoka Iker Casillas Fernández na kutimkia FC Porto mwaka 2015.
Casillas alikaa klabuni hapo kwa tangu mwaka 1998 na aliondoka kwa heshima kubwa baada ya kudaka katika michezo 510.
No comments: