Ommy Dimpoz aeleza jinsi pressure ya kuepuka kutoa ngoma mbovu inavyowapa wasanii mtihani
Hadi unausikia wimbo wa msanii umetoka, kuna vikao vingi hufanyika nyuma ya pazia katika tu kuhakikisha kuwa hatoi wimbo unaoweza kumwaibisha.
Wengi huyapa masikio mengi zaidi ya kuusikiliza wimbo na kutoa maoni kabla ya kuutoa. Hiyo ni moja ya pressure kubwa waliyonayo wasanii kwa sasa hasa waliofanikiwa kwasababu wanahofia kuachia wimbo mbovu lakini pia kutokana na kuwepo kwa ushindani mkubwa.
“Sometimes inakupelekea unaweza kuchukua maoni ya watu 10, pengine katika watu 10, watu 6 au 7 wakakuambia ‘bwana hiki kitu kipo sawa’ lakini bado huamini unaona kama wale watatu kwanini wamekataa,” Ommy Dimpoz ameiambia Bongo5.
“Unaweza ukapata pressure ukaamini wale watu watatu ndio wako sahihi, hawa saba wananipa moyo tu. Kwahiyo unakuwa na pressure kubwa sababu sometimes kuna ngoma inaweza ikatoka, binafsi ukaikubali halafu ukashangaa siku mbili haipo. ‘Hata hii imekataa!’
“Kwahiyo hiyo pressure imekuwa kubwa kiasi kwamba hata mimi mwenyewe nimesema kwamba inakuaje. Lakini mimi ninachoweza kusema ni kwamba kama msanii hutakiwi kulose focus. Na lazima ukubaliane na mambo mawili, unaweza ukatoa nyimbo nzuri ikafanya vibaya lakini haimaanishi kwamba umeisha kisanii, hiyo ipo duniani kote,” ameongeza.
Ommy kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake akiwa na Alikiba.
No comments: