MAKOCHA WAPYA BARCELONA WENGER NDANI.
Baada ya kocha wa Barcelona Luis Enrique kutangaza kubwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu haya ni majina Sita ya makocha waliotwaja kuchukua nafasi yake.
•JORGE SAMPAOLI
Kocha wa aliyewahi kuino timu ya Taifa ya chile raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 56 mwenye mbinu za kiufundi na falsafa ya mashambulizi ya kushtukiza kwasasa Jorge anakinoa kikosi cha Sevilla. Kocha huyo naye amejumuishwa kupewa Dili Catalunya kwakuwa amesema hawezi kusaini mkataba mpya na Sevilla inayoshika nafasi ya tatu akiwa na mchezo mmoja Mkononi nyuma ya Barcelona.
•RONALD KOEMAN
Kocha huyu wa Everton naye amepewa nafasi kubwa ya kukinoa kikosi hicho cha mabingwa wa Hispania. Endapo Barcelona watatamka itabidi waweke fungu la paundi milioni 6.8 kumng’oa kutoka Evertoon.
MAURICIO POCHETTINO
Hii inaweza kuwa njia pekee ya meneja huyo wa Tottenham kurejea La Liga baada ya kipindi kadhaa cha EPL akitokea Soton.
•ERNESTO VALVERDE
Kocha wa Athletic Bilbao Kama akitua Barcelona basi itakuwa ni shinikizo kutoka kwa menejimenti ya juu ya Uongozi wa Barcelona ndiyo inayomtaka aje kurithi nafasi ya Enrique.
•ARSENE WENGER
Anaweza kuondoka Arsenal muda wowote k baada ya zaidi miaka 15 akilisaka kombe la EPL bila mafanikio mahali sahihi ya kwenda kuonyesha ufundi wake ni Barcelona Je Arsene atakubali ulaji huo?
PEP GUARDIOLA
Mashabiki hawana Tatizo naye Catalunya kinachosubiriwa ni mazungumzo yake na wamiliki wa klabu ya Manchester City kama ataamua kuvunja mkataba na kurudi zake Nou Camp.
No comments: