Breaking News
recent

INASEMEKANA “MADARAKA YA KULEVYA” NI DONGO KWA SERIKALI! G NAKO AMEFUNGUKA HAYA!


Baada ya kuachiwa tu kwa ngoma mpya ya kundi la Weusi inayofahamika kama “Madaraka ya Kulevya” wadau wengi wamekuwa wakiihusisha ngoma hiyo na mambo ya kisiasa ambayo yanaendelea nchini kwasasa. Ikiwa ni kutokana na tittle ya ngoma hiyo jinsi inavyo sound na vitu kama hizo.
DJ PAUL24 imeona sio kesi kama itamvuta mmoja kati ya wana wanaoliunda kundi la Weusi na kupiga nae story kuhusiana na ukweli juu ya tetesi hizo za ngoma hiyo kuwa dongo kwa Serikali.
G Nako amekanusha vikali tetesi hizo na kudai kwamba ngoma hiyo ilikuwepo kitambo na wala haina uhusiano hata kidogo na mambo za kisiasa ambazo zinaendelea kwasasa nchini.
“Tunachojaribu kuzungumzia hapa ni mwanamke ambaye umempenda zaidi mwanaume kiasi kwamba mpaka mwanaume huyo anajisahau na kuwa anafanya vitu ambavyo haviendani na matakwa ya mapenzi, ndio ambacho tulijaribu kuzungumza. SIngle hii ilikuwepo kitambo na bado tuna ngoma nyingine na Christian Bella lakini katika uchaguzi watu wameona hii ndio ianze kwenda.” Alisema G Nako.

No comments:


Powered by Blogger.